Wafanyakazi wa Shirika la Usambazaji umeme ( TANESCO) Mkoa
wa Rukwa wakishirikiana na Benki ya NMB wamewatembelea Maafisa wa Magereza wa
Gereza la Molo lililopo Mkoani Rukwa na kutoa elimu inayohusu taratibu za kuunganishiwa huduma ya umeme
kupitia Mradi wa REA awamu ya Tatu.
katika ziara hiyo, Wateja wapatao 96 ambao ni
Wafanyakazi wa Gereza hilo waliweza kuunganishiwa huduma ya
umeme kupitia mradi wa umeme vijijini awamu ya Tatu.
Mbali na kuunganishiwa huduma ya umeme Maafisa hao wa Magereza walipatiwa mafunzo
juu ya namna ya kupata huduma, matumizi sahihi ya kutumia nishati ya umeme, usalama juu ya umeme, ulinzi wa miundombinu ya
umeme na umuhimu wa kutumia umeme ili kuchochea maendeleo Nchi.
Baadhi ya Maafisa wa gereza la Molo wakisikiliza kwa makini
elimu na taratibu za kupata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini REA 3
|
Mkuu wa Gereza la Mollo ACP J.L Mwamgunda,Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja Ndg Lucas C. Kusare na Afisa wa upimaji wakisikiliza maswali kutoka kwa Maofisa wa gereza hilo. |
Afisa Huduma na Mahusiano kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Rukwa
akiwafafanulia maofisa wa Gereza la Molo juu ya utaratibu wa kupata huduma ya
umeme kupitia mradi wa umeme wa REA 3
|
Afisa wa Gereza akiulizia utaratibu wa namna ya kupata
huduma za umeme kupitia Mpango wa REA 3
|
No comments:
Post a Comment