July 4, 2018

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu atembelea mitaa yenye uhitaji wa umeme Kigamboni Jijini Dar Es Salaam


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (katikati), na viongozi wa juu wa TANESCO, wakimsikiliza mtaalamu huyu wakati Mhe. Naibu Waziri alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege kilichoko Kimbiji Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2018.

NA MWANDISHI WETU, KIGAMBONI
NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amefanya ziara ya kukagua miradi ya umeme wilayani Kigamboni ikiwemo ule wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege leo Jumanne Julai 3, 2018.
Ziara hiyo ilimpeleka kwenye mitaa yenye uhitaji wa umeme na kuongea na viongozi na wananchi wa, Minondo, Kimbiji, Mwasonga, Tundwi Songani Pembamnazi, Dege hadi kijiji beach.
Akizungumzia ujio wa Naibu Waziri kwenye eneo hilo la mradi, lililoko Kimbiji, Diwani wa Kata ya Somangila Bw. Chichi Masanja amesema, “Ujio wako Mhe. Naibu Waziri ni faraja kubwa kwetu kwani kero ya umeme mtaa wa Minondo pamoja na Mwanzo Mgumu tuinahakika ziara yako itatia chachu ya mradi kukamilika na kiro hii kufika mwisho.” Alisema Diwani huyo Bw. Masanja.
"Kuja kwetu mara kwa mara wilayani Kigamboni kunatokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme kwenye eneo hili, lakini Serikali tunayo nia ya dhati ya kuhakikisha wakazi wa Kigamboni wanapata umeme wa uhakika ndio maana tumejenga vituo vya kupoza na kusambaza umeme kule Tungi, Mbagala, Kurasini, na kituo hiki cha Kurasini kitapitisha miundombinu Baharini ili kuunganisha Sub-Station ya Dege ili sasa kuwezesha eneo hili kuwa na umeme wa uhakika." Alisema Mhe. Subira Mgalu.
Mhe. Naibu Waziri aliwapongeza wananchi kwa kupisha ujenzi wa msongo wa umeme wa 132kV.
"Hapo awali Kigamboni idadi ya watu ilkikuwa ndogo, lakini kwa sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu na hivyo uhitaji wa umeme umekuwa mkubwa na sisi Wizara ya Nishati kupitia TANESCO tunawiwa kusimamia miradi hii ikamilike kwa haraka." Alisema.
Naibu Waziri alisema, Sekta ya Nishati ni sekta wezeshi na jambo lolote la kimkakati linafanikiwa kwa uwepo wa nishati ya uhakika na kwa gharama nafuu na kwakweli kuja kwetu hapa ni jitihada za kuhakikisha changamoyo hiyo ya umeme inafika mwisho.

Tayari ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege unaendelea kwa kasi ambapo hadi sasa makandarasi wazawa kutoka TANESCO wameshajenga sakafu ya kufunga mashine ikiwa ni pamoja na eneo lote la mardi kuzungushiwa uzio kama ilivyoagizwa na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo hilo kwa mara ya kwanza Agosti 22, 2017 ambapo eneo hilo lilikuwa pori tu.
Katika ziara hiyo Mhe. Mgalu alifuatana na Naibu Mkurugenzi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji (Power
Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa pamoja na Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya.

Hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Dege kilichoko Kimbiji Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam. Eneo hilo lilikuwa pori tu mwishoni mwa mwaka jana, ambapo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, aliagiza pajengwe uzio na kasi ya ujezni iongezeke.
Mhe. Subira Mgalu (katikati) akiwa na Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya (kulia) na Diwani wa Kata ya Somangila Bw.Chichi Masanja.
Wananchi wa Golani wakitoa kero zao.
Mhe. Naibu Waziri akiorodhesha maoni ya wananchi.

Mkazi wa Mtaa wa Minondo, akitoa maoni yake.


No comments:

Post a Comment