November 26, 2013

KANUSHO LA BEI YA UMEME

TAARIFA KWA UMMA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linakanusha vikali taarifa iliyoandikwa katika baadhi ya magazeti kwamba Serikali imepandisha bei ya umeme.
Ukweli ni kwamba TANESCO bado haijapandisha bei ya umeme ila imepeleka maombi ya kuomba kuongeza bei ya umeme kwa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) na si serikali.
Tunapenda kusisitiza kwamba TANESCO iko tayari kutoa majibu wakati wowote endapo waandishi wa habari wanahitaji kuelewa ama kupata ufafanuzi juu ya masuala ya umeme na shirika kwa ujumla kupitia katika ofisi ya Mawasiliano iliyopo Ubungo Makao Makuu au simu namba +255 222 451 185, barua pepe communications.manager@tanesco.co.tz, twitter.com/tanescoyetu na umemeforum.blogspot.com

2 comments:

  1. MNAHITAJI KUONGEZA GHALAMA KWA KIASI GANI?

    ReplyDelete
  2. Jamani tunateswa na mgao wa umeme walitangaza siiu kumi sasa wanaendelea jamani aibu na shida gani hii Tanzania

    ReplyDelete