ULIPAJI WA FIDIA KWA WAHANGA WANAOPITIWA NA MRADI
Kilwa
Energy kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wana
mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Somanga
Mtama mpaka Kinyerezi.
Wananchi
waliopitiwa na Mradi huu wanaombwa kurejea tangazo lililotolewa tarehe
01-08-2013 kwenye magazeti mbalimbali kuhusu ulipwaji wa fidia na kwamba
malipo ya fidia yalitarajiwa kuanza kulipwa
tarehe 30-11-2013. Kutokana na sababu mbalimbali tunasikitika kutoa
taarifa kuwa zoezi hilo halitaanza kama lilivyotarajiwa.
Katika
kipindi hicho baadhi ya mikataba muhimu inayohitajika kati ya Kilwa
Energy, Serikali, na TANESCO ilikamilika na pia kukamilisha makabrasha
ya fidia. Kwa sasa Kilwa Energy imetuma maombi serikalini
kuomba kukamilisha mikataba yote iliyosalia na pia wanawasiliana na
wafadhili mbalimbali kuona uwezekano wa kukamilisha mikataba hiyo mapema
iwezekanavyo.
Zoezi la kuhakiki majina na ufunguzi wa akaunti ulisitishwa ili taratibu za mikataba iliyosalia ikamilike.
Ili kuokoa
muda na kuharakisha zoezi zima wakati utaratibu wa kukamilisha mikataba
unaendelea, Kilwa Energy na TANESCO wataendelea na zoezi la
1. Kuhakiki majina
ya wananchi wote wanaopitiwa na mradi kwa kupiga picha na kujaza fomu
maalum itakayokuwa inaonesha malipo stahiki.
Wananchi watajulishwa lini zoezi la ulipaji fidia litaanza kupitia vyombo vya habari.
Kilwa
Energy na TANESCO linawaomba tena wananchi wote wanaopitiwa na Mradi huu
kuwa wavumilivu wakati huu wa ukamilishaji wa mikataba iliyobaki. Hivyo
basi, tunatarajia mara tu mikataba hiyo itakapokamilika
malipo yatashughulikiwa.
Kilwa Energy na TANESCO wanaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
IMETOLEWA KWA USHIRIKIANO WA WAKURUGENZI WATENDAJI WA KILWA ENERGY NA TANESCO
Mimi ni mhanga Wa mradi huu na ningependa kujua lini hasa fidia italipwa?
ReplyDeletesuala hili limekuwa la muda mrefu sana na hatujuia litakwisha lini. Naomba kujulishwa hatua iliyofikiwa ikiwa ni pamoja na lini malipo yetu yatafanyika? Mimi ni mmoja wa wahanga wa mradi huo.Nashauri taarifa zitolewe kupitia vyombo vya habari na sio kukaa kimya.
ReplyDelete