TAARIFA KWA UMMA
Wakati
matengenezo ya kiufundi katika visima vya gesi vilivyopo katika kisiwa
cha Songosongo, wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi yakiendelea na kusababisha
upungufu wa umeme katika gridi ya taifa, Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), linawaomba wateja wake wenye viwanda na migodi kusitisha
matumizi ya umeme nyakati za usiku na kuendelea kutumia umeme nyakati za
mchana tu ili umeme uweze kutosheleza wateja wa
majumbani katika kipindi cha usiku.
Zoezi
hili ni la muda mfupi kuanzia sasa hadi Novemba 26, mwaka huu ambapo
matengenezo ya kiufundi katika visima hivyo vya gesi yatakuwa
yamekamilika
na umeme kurejea katika hali ya kawaida.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU
Tanesco
ReplyDeleteDont you think such maintenance should be done during the cool months like June/July to spare Dar Residents of scorching heat? can you use gas only for few months to let water build up in dams and use hydro during such days when gas is not available?