June 26, 2015

TAARIFA

         TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa kuna watu wanatumia jina la TANESCO vibaya katika mitandao ya kijamii (facebook na twitter)kujibu watu matusi,kulikashifu shirika na kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu shirika kwa kujifanya wao ni TANESCO.

Shirika limeshatoa taarifa Mamlaka ya udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuwasiliana na vyombo vingine vya usalama juu ya uhujumu huo.Mitandao hiyo ina akaunti za facebook zinasomeka (TANESCO TZ  na TANESCO)na akaunti za twitter zinasomeka (Tanesco@TANESCO-,Tanesco Escober@tanescobar,TANESCO LTD@tanesco-)

Tanesco inaendelea kuzikana akaunti hizo na kwamba chochote kinachoandikwa huko si msimamo au maelezo kutoka shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).Mitandao sahii ya TANESCO ni :
Facebook:www.facebook.com/tanescoyetu.
Twitter:www.twitter.com/@tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi wateja wake kwa usumbufu wowote walioupata kutokana na upotoshwaji wa taarifa kwanye mitandao hiyo.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment