Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi kuhusu masuala muhimu ya TANESCO. Wengine pichani, kulia ni Meneja wa Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano wa Shirika hilo, Leila Muhaji.
NA MAGRETH SUBI
SERIKALI
kupitia TANESCO imefanya uwekezaji mkubwa kwenye Miradi mbalimbali ya Umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni 5.35, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba amewaambia waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Novemba 24, 2016.
Akitoa
ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika la Umeme Nchini, Mhandisi Mramba
alisema, “Katika historia ya Sekta ya Umeme, haijawahi kutokea uwekezaji mkubwa
kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi yote ya Umeme inayoendelea
na ambayo tayari imetengewa fedha ina thamani ya Shilingi Trilioni 3.85, na
majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa
Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi
Mramba.
“
Uwekezaji huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na
vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.
Mhandisi
Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa upanuzi wa
Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania, TEDAP,
Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es
Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi na Rusumo Power Plant
(T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.
Akifafanua
zaidi kuhusu uwekezji huo, Mkurugenzi Mtendaji alisema, Miradi yote ambayo thamani
yake imetajwa haihusishi Miradi ya usambazaji umeme Vijijini chini ya mpango wa
REA.
Akizungumzia
utaratibu mpya wa manunuzi,(Procumbent), Mhandisi Mramba alisema, TANESCO
imechukua hatua kadhaa ili kuboresha manunuzi ambapo kuanzia sasa makampuni
yanayomilikiwa na mtu mmoja kuhodhi manunuzi ya Shirika hilo, na kwamba zabuni
zote zilizotangazwa kuanzia mwaka huu wa fedha, haitaruhusiwa kampuni moja kuwa
na mikataba miwili kwa wakati mmoja.
Akifafanua
zaidi alisema, Katika zabuni moja haitaruhusiwa kampuni moja kupewa zaidi ya
Lot 1, “Hii imeanza kusaidia kuondoa ukiritimba katika manunuzi na kuwapa
Watanzania wengi zaidi nafasi pana ya kushiriki katika zabuni za kusambaza
vifaa vya umeme.” Alifafanua Mhandisi Mramba.
Aidha
Mhandisi Mramba alisema, ili kuwezesha Watanzania wengi kushiriki katika uchumi
wa nchi, TANESCO itanunua vifaa vya umeme vinavyozalishwa hapa nchini na
kuachana na mtindo wa kuagiza kutoka nje.
“Mfano
kwa nguzo za umeme tumewapa Sao Hill, ambao watatuuzia nguzo 96,500, na new
Forest watatuuzia nguzo za umeme 9,668, na kwa upande wa Transfoma za umeme,
kandarasi hiyo imepewa kampuni ya TANELEC itakayotuuzia transfoma 1,500”
Alifafanua
Akieleza
zaidi kuhusu ununuzi wa vifaa, Mhandisi Mramba alisema, kampuni ya East Africa
Cables, intarajiwa kupewa kazi ya kusambaza waya na kuongeza kuwa utaratibu huo
pia utatumika kwenye huduma nyingine kama vile Bima, ambapo alisema Shirika
linatarajia kulitumia Shirika la Bima la Taifa, (NIC), kutoa huduma hiyo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya umeme, Mhandisi Mramba aliwahakikishia Watanzania kuwa kutokana
na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika hilo katika kuboresha miundombinu ya
umeme, hakutakuwa na mgao wa umeme nchini na ndio maana kwa muda mrefu sasa
hakuna mgao wa umeme.“Mwaka 2015 nchi ilikuwa na mgao wa umeme wa jumla ya
MW300, na maeneo mengine yalikuwa na hali mbaya hususan Mwanza, Arusha na Kilimanjarolakini
kwa sasa hali ya umeme katika mikoa yote na mingine ni nzuri hakuna mgao na
kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa
muda mfupi.” Alisema.
Hata
hivyo alisema Shirika lake linaongeza juhudi za kusambaza umeme kwa watanzania
wengi zaidi kote nchini, kutokana na uwekezaji wa miundombinu unaoendela kila
kona ya nchi.
Mhandisi
Mramba aliwaondoa wasiwasi wananchi kuhusu ombi la Shirika hilo la kuongeza
asilimia 18.9 ya bei ya umeme kuanzia Januari mwakani, kwa kusema ongezeko hilo
halitaathiri watumiji wa kawaida majumbani. “Tunachoomba kutoka kwa Msimamizi
(Regulator), ni kufanya mabadiliko ya kutenganisha watumiaji umeme wa majumbani
na wale wanaotumia kibiashara kama vile mabango ya matangazo, kwani hivi sasa
wote wanalipa gharama sawa na hili si sawa.” Alisema.
Aliwaasa
wananchi kuridhia ongezeko hilo kwani Shirika limo katika jitihada kubwa za kuhakikisha
Wananchi wengi zaidi wanapatiwa umeme kwa kufikisha miundombinu ya umeme kwenye
maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo gharama za kufanya hivyo zimeongezeka.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo
No comments:
Post a Comment