November 2, 2016

UBORESHWAJI WA KITUO KIKUBWA CHA UMEME ILALA PAMOJA NA NJIA YA CHINI YENYE MSONGO MKUBWA WA UMEME                                 SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)UBORESHWAJI WA KITUO KIKUBWA CHA UMEME  ILALA PAMOJA
          NA NJIA YA CHINI YENYE MSONGO MKUBWA WA UMEME


Shirika la Umeme Tanzania TANESCO  linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala  na Temeke  kuwa kutakuwa na uboreshwaji wa Kituo kikubwa cha umeme Ilala na njia kubwa ya kusafirisha umeme chini ya ardhi Jumamosi Novemba 05, 2016 kuanzia SAA 3:00 Asubuhi hadi SAA 06:00 Mchana.

Kutokana na maboresho hayo, Kituo cha Kupoza na Kusafirisha umeme cha Ilala kitazimwa na maeneo yote ya kati kati ya jiji, Upanga, Kariaokoo, Buguruni, Ilala, Wizara ya maliasili na utalii, Keko Mwanga, Maeneo ya Bandari, Mbagala, Kijichi, Kurasini na maeneo ya jirani yatakosa umeme.


Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Kwa Huduma za Dharura piga;-Dawati Letu la Huduma za Dharura Ilala:
022 213 3330, 0784 768586, 0715 76 85 86, Temeke:- 0712 052720, 022 2138352 AU Huduma ya Miito ya Simu 2194400 or 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


IMETOLEWA NA:-OFISI YA UHUSIANO
                                   TANESCO MAKAO – MAKUU.


No comments:

Post a Comment