November 6, 2016

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO MHANDISI FELCHESMI MRAMBA, ATEMBELEA VITUO VIPYA VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VYA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam

NA Grace Kisyombe
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupoza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.
Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.
Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.

“Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha katikati ya jiji.
Mhandisi Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.” Alitoa hakikisho.

Maboresgho hayoyalihusisha ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupoozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema,

Alisema, ujenzi wa mfumo huo wa njia ya umeme wa ardhini (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 ni kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City
“Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika ulio kwenye viwango stahiki,

Naye Meneja Mwandamizi wa Miradi yausafirishaji na usambazaji umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Geirge Chegere, alimueleza Mhandisi Mramba kuwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.
Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuriya Muunganowa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, baadaye mwezi huu wa Novemba.




Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa  Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.akielezea hatuailiyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam

 Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, akielezea teknolojia ya kisasa ya mashine ndogo yenye kufanya kazi kubwa
 Kituo cha City Centre
 Mhandisi Mramba, akitembelea mitamboya kituo cha City Centre
 Fundi mitambo ya umeme akiwa kazini kituo cha Ilala Mchikichini
 Mhandisi Mramba, (kushoto), akizungumza wakati alipotembelea kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini kujionea maendeleo yaujenzi wa kituo hicho
 Mitambo ya kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Kurasini
 Mhandisi Chegere (wapili kulia), akipatiwa maelezo ya mitambo ya kituo cha City Centre
 Jengojipya la kituo cha Ilala Mchikichini
 moja ya mashine mpya kituo cha Ilala Mchikichini
 Chumba cha mitambo mipya ya umeme kituo cha Ilala Mchikichini
 Mhandisi Mramba, akiwa na wahandisiwenzake, Chegere (kulia) na Mgaya, kwenye kituo cha City Centre
Mitambomipya kituo cha Kurasini

No comments:

Post a Comment