January 29, 2018
Mhe. Mgalu akagua Miradi ya REA Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Subira Mgalu amekagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Pili na Tatu (REA PHASE II & III) Mkoani Kilimanjaro wenye jumla ya Vijiji 18 katika Wilaya za Rombo, Mwanga na Same.
Aidha, Mhe. Mgalu alitumia ziara hiyo kuwatambulisha Wakandarasi kwa Wananchi na kuwataka kutokurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.
Pia alitembelea Bwawa la kuzalisha umeme la Nyumba ya Mungu kujioneo shughuli za uzalisha.
Mhe. Mgalu alikamilisha ziara hiyo Mkoani Kilimanjaro Januari 26, 2018.
January 25, 2018
TANESCO yaboresha Huduma kupitia Mfumo mpya wa GIS
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuboresha huduma zake kwa Wateja kwa kubuni na kuanzisha mfumo mpya wa kiteknolojia utakaokusanya na kujumuisha taarifa zotemuhimu za miundombinu ya umeme na Wateja kupitia mfumo wa GIS (Geographical Information System).
Mfumo huu unaambatana na ramani ya miundombinu ya umeme na makazi ya Wateja, ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia Wataalamu na kutoa huduma kwa muda mfupi na kwa haraka zaidi.
Dkt. Mwinuka afanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka amefanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2018.
Ikiwa ni kikao chake cha kwanza kukutana na Wafanyakazi tangu kuteuliwa kwake.
Dkt. Mwinuka alisema kukutana kati ya Uongozi na Wafanyakazi kunapunguza "Gape" na kuondoa malalamiko.
Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Wafanyakazi wa TANESCO kwa kufanya kazi nzuri mwaka uliopita wa 2017 kwani kwa kiasi kikubwa malalamiko ya Wateja kwa Mkoa huo yalipungua na pia Mkoa wa Morogoroulitekeleza vizuri Operesheni ya KA - TA.
Akizungumzia hali ya kifedha ndani ya Shirika aliwataka Wafanyakazi kushiriki kila mmoja kuboresha kwa nafasi yake, kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kwa upaande wa vifaa vitoke stoo kwa mahesabu mazuri.
"Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wa TANESCO ni waaminifu na wachapa kazi, lakini hao wachache wanaohujumu waache ili Wafanyakazi wote tuwe waaminifu". Alisema Dkt. Mwinuka.
Aliwataka Wafanyakazi kuongeza nguvu zaidi ili kufikia malengo.
Wafanyakazi walitoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali ambayo Uongozi uliyatolea ufafanuzi, na yaliyo yalihitaji utekelezaji uliyapokea.
January 23, 2018
Dkt. Kalemani akagua maendeleo ya maandalizi ujenzi Mradi wa Stiegler's Gorge
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya maandalizi ujenzi wa Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge ikiwemo njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 33 kutoka Msamvu hadi mto Rufiji.
Njia hiyo ya umeme inajengwa na Kampuni Tanzu ya TANESCO ETDCO.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa Mradi wa Stiegler's Gorge unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi Februari mwaka huu baada ya Mkandarasi kupatikana.
Dkt. Kalemani alisema katika utekelezaji wa Mradi huo Vijiji viwili vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme kwa bei ile ile ya umeme Vijijini (REA).
"Moja ya matayarisho ya utekelezaji ni ujenzi wa njia ya umeme utakaowawezesha Wakandarasi kupata umeme wakati wa ujenzi". Alisema Dkt. Kalemani.
Aliongeza katika utekelezaji Wizara tatu zinashirikiana ambazo ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Miundombinu na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mradi huo unaotarajiwa kuchukua miaka miwili hadi mitatu mpaka kukamilika kwake baada ya Mkandarasi kuwa ameanza kazi.
Aidha, Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia miamoja.
Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme nchini Dkt. Kalemani alisema hivi sasa imeimarika tofauti na mwezi Novemba ambapo kulikuwa na ukkarabati mkubwa wa mitambo katika Vituo vya kuzalisha umeme.
Aliwataka Wananchi kusaidia kutoa taarifa panapotokea hitilafu ili ziweze kurekebishwa kwa haraka.
"Tutaendelea kukarabati miundombinu ya umeme ili kuimarisha hali ya upatikanaji umeme".Alisisitiza Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliomba kwa Mhe. Waziri Wizara ya Maji ishirikishwe pia katika Mradi huo kusaidia vijiji unaopiti
January 10, 2018
TANESCO yawashukuru Wateja kwa mchango mkubwa mwaka 2017
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka
amewashukuru Wateja, wanahabari na wadau wote kutokana na mchango mkubwa kwa
Shirika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ambazo zimeisaidia TANESCO katika kuboresha huduma zake.
Aidha, amesema hali ya uzalishaji umeme unaendelea vizuri kutokana na
kuanza kufanya kazi kwa mashine mbili kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha
Kinyerezi II, kukamilika kwa ukarabati wa mashine ya kufua umeme Kidatu, na
kuongezeka kwa kina cha maji kwenye bwawa la Mtera, kuimarika huku kumepelekea TANESCO kuwa na umeme wa ziada.
Akizungumzia njia za kusafirisha umeme, alisema ukarabati wa
miundombinu unaendelea katika njia za kusafirisha umeme.
“Suala la kukatika kwa umeme Kigamboni, ufumbuzi wake
utapatikana baada ya kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti
132 ambapo njia hiyo imefika kituo kipya cha Mbagala”. Alisema Dkt. Mwinuka.
Aliongeza hivi sasa Kigamboni inatumia umeme kutoka njia ya
umeme ya kilovolti 32 ya Kipawa – Chang’ombe ambayo pia inatumiwa na Viwanda.
Alisema, licha ya mvua kuwa na changamoto ya uharibifu wa
miundombinu ya umeme lakini inafaida kwa TANESCO katika mabwawa kwani
inachangia asilimia 41.5.
January 7, 2018
Waziri Mkuu: “Umeme ni fedha, Kuwepo kwa Umeme ni Ajira tosha”
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma
ameweka jiwe la msingi la mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa
kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na ujenzi wa jengo la Ofisi
ya TANESCO Mkoani Ruvuma.
Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la ziara hiyo ni
kuwatayarisha Wananchi juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na
Serikali huku akieleza msimamo wa Serikali ni maslahi ya nchi kwanza.
Aliongeza, mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano
katika Sekta ya Nishati, ni kuona mtandao wa umeme unaenea pote nchini, na katika Vijiji ambavyo ni vigumu kufikika
kwa miundombinu ya umeme Vijiji hivyo vitatumia umeme wa jua (Solar System).
Ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi TANESCO kupitia kwa
Mwenyekiti wake Dkt. Alexander Kyaruzi, Menejimenti ya TANESCO pamoja na
Wafanyakazi kwa kuunga mkono katika utekelezaji wa Sera za Serikali.
“Nimpongeze Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa namna Bodi inavyosimamia, hongera sana wana
TANESCO kwa kuunga mkono jitihada za Serikali”. Alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, alisema amefarijika sana kwa kuhakikishiwa ujenzi
wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea kukamilika mwishoni
mwa mwezi Agosti na jingo la Ofisi mwezi Machi mwaka huu.
Aliongeza kufika kwa umeme wa gridi kutafungua fursa
za kibiashara kwa Wananchi wa maeneo hayo hivyo kutokuwepo malalamiko ya
ukosefu wa ajira kwa watu kujiari, “Ndugu zangu Umeme ni fedha, Kuwepo kwa
Umeme ni Ajira tosha, hivyo tuwekeze katika biashara ndogo ndogo za kutuingizia
kipato”.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani alisema katika kipindi cha Miaka miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa
na mafanikio katika sekta ya nishati nchini ambapo katika njia za kusafirisha
umeme mkubwa zimejengwa mbili ambazo ni mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa
kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga na mmradi wa njia ya kusafirisha
umeme wa kilovolti 220 kutoka Makambako Mkoani Njombe hadi Songea Mkoani Ruvuma wenye urefu wa
kilometa 250.
Aliongeza kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme
ya Makambako hadi Songea kutaipunguzia TANESCO gharama kwa kuacha kutumia mitambo
ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta katika vituo vya Songea, Mbinga Namtumbo
na Madaba .
January 4, 2018
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WATEJA WALIOHAMISHWA KUTOKA MITA ZA ZAMANI KWENDA LUKU WAKIWA NA MADENI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunawataarifu Wateja wetu wenye madeni, ambao walihamishwa kutoka mita za zamani (Conversional Metter) kwenda mita za LUKU kuwa,
Hapo awali walipokuwa wakifanya manunuzi ya umeme, nusu
ya fedha ilikatwa kulipa deni la umeme, TANESCO sasa imebadilisha, na kuweka mfumo mfumo ambao utawezesha madeni
hayo kumalizika ndani ya miaka miwili (2).
Kwa wale ambao madeni yalitokana na wizi wa umeme
yanatakiwa yakamilike ndani ya miezi sita (6).
Kwa mawasiliano toa taarifa kupitia,
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400
na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz,
mitandao ya kijamii: Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
IMETOLEWA
NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO
MAKUU
JANUARI 04,
2018
Subscribe to:
Posts (Atom)