Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya maandalizi ujenzi wa Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge ikiwemo njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 33 kutoka Msamvu hadi mto Rufiji.
Njia hiyo ya umeme inajengwa na Kampuni Tanzu ya TANESCO ETDCO.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa Mradi wa Stiegler's Gorge unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi Februari mwaka huu baada ya Mkandarasi kupatikana.
Dkt. Kalemani alisema katika utekelezaji wa Mradi huo Vijiji viwili vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme kwa bei ile ile ya umeme Vijijini (REA).
"Moja ya matayarisho ya utekelezaji ni ujenzi wa njia ya umeme utakaowawezesha Wakandarasi kupata umeme wakati wa ujenzi". Alisema Dkt. Kalemani.
Aliongeza katika utekelezaji Wizara tatu zinashirikiana ambazo ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Miundombinu na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mradi huo unaotarajiwa kuchukua miaka miwili hadi mitatu mpaka kukamilika kwake baada ya Mkandarasi kuwa ameanza kazi.
Aidha, Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia miamoja.
Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme nchini Dkt. Kalemani alisema hivi sasa imeimarika tofauti na mwezi Novemba ambapo kulikuwa na ukkarabati mkubwa wa mitambo katika Vituo vya kuzalisha umeme.
Aliwataka Wananchi kusaidia kutoa taarifa panapotokea hitilafu ili ziweze kurekebishwa kwa haraka.
"Tutaendelea kukarabati miundombinu ya umeme ili kuimarisha hali ya upatikanaji umeme".Alisisitiza Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliomba kwa Mhe. Waziri Wizara ya Maji ishirikishwe pia katika Mradi huo kusaidia vijiji unaopiti
No comments:
Post a Comment