Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka
amewashukuru Wateja, wanahabari na wadau wote kutokana na mchango mkubwa kwa
Shirika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ambazo zimeisaidia TANESCO katika kuboresha huduma zake.
Aidha, amesema hali ya uzalishaji umeme unaendelea vizuri kutokana na
kuanza kufanya kazi kwa mashine mbili kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha
Kinyerezi II, kukamilika kwa ukarabati wa mashine ya kufua umeme Kidatu, na
kuongezeka kwa kina cha maji kwenye bwawa la Mtera, kuimarika huku kumepelekea TANESCO kuwa na umeme wa ziada.
Akizungumzia njia za kusafirisha umeme, alisema ukarabati wa
miundombinu unaendelea katika njia za kusafirisha umeme.
“Suala la kukatika kwa umeme Kigamboni, ufumbuzi wake
utapatikana baada ya kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti
132 ambapo njia hiyo imefika kituo kipya cha Mbagala”. Alisema Dkt. Mwinuka.
Aliongeza hivi sasa Kigamboni inatumia umeme kutoka njia ya
umeme ya kilovolti 32 ya Kipawa – Chang’ombe ambayo pia inatumiwa na Viwanda.
Alisema, licha ya mvua kuwa na changamoto ya uharibifu wa
miundombinu ya umeme lakini inafaida kwa TANESCO katika mabwawa kwani
inachangia asilimia 41.5.
No comments:
Post a Comment