March 17, 2014

HUDUMA MPYA

KUANZA KWA HUDUMA YA KUWATUMIA WATEJA BILI KWENYE SIMU ZA MKONONI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika kuhakikisha kuwa linaboresha huduma zake, linatarajia kuanzisha huduma ya kuwatumia wateja wake bili za kila mwezi kwenye simu zao za mkononi kwa wateja wanaotumia mita za kulipia umeme baada ya kutumia.
Mfumo huu umelenga kurahisisha upatikanaji wa bili za wateja kwa uharaka zaidi na pia kuondoa usumbufu kwa wateja kulazimika kufuata bili zao katika ofisi za TANESCO au katika masanduku ya barua.
Hivyo basi uongozi wa Shirika unawaomba wateja wake wote wenye mita za kulipia baada ya kutumia “Conventional au Post Paid Meters” kuorodhesha majina yao kamili, namba za simu za mkononi na namba za mita kwenye ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu.
Ushirikiano wa wateja wetu utasaidia kufanikisha zoezi hili.
“TANESCO Tunayaangaza Maisha Yako”
SIMU: +255 022 2451130/38:  Fax +255 022 2451148
HUDUMA KWA WATEJA +255 768 100:  022 219 4400
BARUA PEPE:customer.service@tanesco.co.tz.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu

No comments:

Post a Comment