January 5, 2015

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINIShirika la umeme Tannania (TANESCO) linapenda kuwataarifu  wateja wake kuwa kesho Jumanne tarehe 06/01/2015 kituo cha kupooza umeme cha MASAKI kitazimwa ili kupisha matengenezo ikiwa pamoja na kukata miti iliyo chini ya laini.Katizo hili litakuwa kati ya saa 3:00 asubuhi na saa 11:00 jioni
Maeneo yatakayoathirika ni; Eneo lote la Masaki ikiwemo balozi za Falme za kiarabu na Afrika Kusini, makazi ya balozi wa Canada na Ujerumani,hoteli za Sea Cliff, Oysterbay, Alexander, Slip way, Golden tulip, Mzinga way,Mitaa ya Mwaya, Chole ,Mahando ,Katoke,Mahenge,Uganda,Mawenzi,Toure, Mlale,TPDF Masaki mwisho,Bandari quorters,NASACO flats,Kahama mining,Valahala village,UNDP quorters,Baobao village,IFM flats,Muhimbili (MUHAS) university hostel,Kipepeo apartments,
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu

No comments:

Post a Comment