January 27, 2014

KINONDONI KASKAZINI

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME LEO MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaaomba radhi  wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kutokana na  katizo la umeme la dharura, lililotokea Usiku wa kuamkia leo Januari 27, 2014 majira ya saa 9 alfajiri.
Sababu kubwa ilikuwa ni kuungua ghafla kifaa cha kukata umeme cha msongo wa Kilovolti 33 kwenye Kituo cha Tegeta.
Maeneo yaliyokuwa yameathirika ni Mwenge, Lugalo, Bahari Beach, Tegeta, Wazo, Boko na maeneo ya jirani.
Umeme ulirejejeshwa kwenye hali ya kawaida kuanzia saa 6.20 mchana na hadi kufikia saa 8.30 alasiri maeneo yote yalikuwa yanapata umeme.
Uongozi unasikitika na unaomba radhi kwa kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na:    
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAOKA MAKUU.

No comments:

Post a Comment