Kufuatia janga la mafuriko lililoyakumba baadhi ya maeneo ya
Jiji la Dar es salaam miezi miwili iliyopita na Serikali kuamua kuwapatia
waathirika maeneo salama ya makazi katika kijiji cha Mabwepande nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Tarehe 13 Januari, Mh. Rais Jakaya Kikwete, aliomba Taasisi zote zinazotoa huduma muhimu kama Maji, Barabara na Umeme, kutoa ahadi ya lini watafikisha huduma hizo haraka. Meneja Mahusiano wa Tanesco,Bi. Badra Masoud ambaye alimwakilisha,Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mwandisi William Mhando, kwakutambua umuhimu wa huduma ya umeme kwa waathirika, , alitoa ahadi ya siki 14 kumaliza kuweka miundombinu ya umeme. Kikosi maalumu cha kukarabati umeme Dar es Salaam (KAUDA) walikabidhiwa jukumu ilo.
Hatimaye tarehe 05, Feb tumeweza kufikisha umeme kwenye viunga vyote vya makazi mapya ya Mabwepande. Meneja Mahusiano, Bi. Badra Masoud ametembelea maeneo ya ujenzi wa mradi na kushuhudia ujenzi umekwisha na taa chache zilizowekwa kwenye nguzo.
Ndipo Uongozi wa Shirika wakaamua kuwapongeza KAUDA
kuonyesha kutambua kazi ngumu waliyoitekeleza , lakini pia kupata nafasi ya kusikia toka kwao.
Mafundi wa KAUDA wakipata chakula katika tafrija
ya kuwapongeza
|
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, William Mhando akipata chakula cha jioni, pamoja na mafundi wa KAUDA. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,. Mhandisi, William Mhando akiwapongeza mafundi wa KAUDA kwa kupita katika meza zao |
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, William Mhando akiwa katika picha ya pamoja na mafundi wa KAUDA. |
No comments:
Post a Comment