Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud alipotembelea Makazi ya waathirika wa Mafuriko , Mabwepande. |
Hatimaye Tanesco imekuwa taasisi ya kwanza kumaliza kuweka miundombinu
mipya ya umeme kwa waathirika wa mafuriko waliopewa makazi mapya Mabwepande.
Kufuatia janga la mafuriko lilitokea sehemu kadhaa za viunga vya Mji wa Dar Es
Salaam na Serikali kuamua kuwahamishia wakazi wote waliokuwa katika maeneo hayo
hatari kwa kuwapatia maeneo nje kidogo ya mji, Mabwepande kuwa makazi yao mapya
na ya kudumu.
Kufuatia uzito wa tatizo ili Mh. Rais Jakaya Kikwete alikutana na
wawakilisha wa taasisi muhimu za Serikali kuona jinsi ya kujenga miundombinu
haraka katika maeneo ya Mabwepande ili waathirika waweze kuishi maisha salama
na ya kawaida. TANESCO ikiwakilishwa na Meneja Mahusiano Bi, Badra Masoud.
Tarehe 13 Januari, Rais aliomba Taasisi zote zilizotakiwa kujenda
miundombino kama Maji, Barabara na Umeme, kutoa ahadi ya lini watafikisha
huduma hizo za dharura. Meneja Mahusiano Tanesco,Bi. Badra Masoud ambaye
alimwakilisha,Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mwandisi William Mhando, kwakutambua
umuhimu wa huduma ya umeme kwa waathirika, , alitoa ahadi ya siki 14 kumaliza
kuweka miundombinu ya umeme. Kikosi
maalumu cha kukarabati umeme Dar es Salaam (KAUDA) walikabidhiwa jukumu ilo.
KAUDA baada ya kukabidhiwa ramani ya ujenzi wa makazi hayo, tarehe 16
walianza kazi rasmi ya kuweka miundombinu ya umeme. Kwasababu ya ukubwa wa eneo
na uharaka wa mradi huu, ulifanya kazi ya ujenzi kuwa ngumu sana na kuwafanya
KAUDA kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanatimiza ahadi ya
kufikisha umeme kwa siku 14 tu.
Hatimaye tarehe 05, Feb Tumeweza kufikisha umeme kwenye viunga vyote vya
makazi mapya ya Mabwepande. Meneja Mahusiano, Bi. Badra Masoud ametembelea
maeneo ya ujenzi wa mradi na kushuhudia ujenzi umekwisha na taa chache zilizowekwa
kwenye nguzo zikiwaka.
Badra Masoud akionyesha mwenye furaha kubwa, aliwapongeza mafundi wa kikosi maalumu cha Tanesco
(KAUDA), kwa kazi nzuri.
Transifoma inayopoza umeme tayari kwa kugawa umeme,
na Taa kubwa kusaidia kangaza makazi
|
“ Nyie ni kikosi chetu cha kujivunia, nawashukuru sana kwa kazi nzuri,
natambua ugumu wa kazi hii, hata nilipokuwa natoa ahadi mwenyewe nilitia shaka
lakini niseme mumetupa heshima kubwa kama shirika”
“TANESCO INAYAANGAZA MAISHA YAKO”
No comments:
Post a Comment