Shirika la Umeme
Tanzania – TANESCO linapenda kuwaomba
radhi wateja wake wote wanaoishi maeneo ya Gongo la mboto, Ukonga, Segerea, Moshi
Bar, Kipunguni, Mazizini, Kisarawe, Pugu
Mikongeni,Pugu Kajiungeni,Chanika,Markaz,Chuo Cha Kampala, Ukonga Magereza, Majohe,
Kiwanda cha Namera, Tabata Kisiwani, Tabata Kisukulu, Bonyokwa, Tabata Segerea,
Tabata Kinyerezi, Tabata Bima, Tabata Chang’ombe, Karakata, Stakishari, Kisarawe
na baadhi ya Maeneo ya viwanda vilivyopo
kandokando ya barabara ya Mandela hadi Mwananchi kutokana na tatizo la
kukatikakatika kwa umeme kwenye maeneo hayo.
Tatizo hilo
limesababishwa na kuharibika kwa transfoma kubwa iliyoko katika kituo chetu cha
umeme cha Kipawa iliyokuwa inasambaza umeme kwenye maeneo hayo.Tatizo hilo
lilipelekea kutumia njia mbadala ya kusambazia umeme ya kutoka Ubungo badala ya
ile ya awali ya Kipawa ambayo kuanzia mwezi wa Januari, 2012 hadi sasa imezidiwa
kutokana na ongezeko kubwa la matumizi ya umeme. Mikakati ya dharura ya
kulishughulikia tatizo hilo inaendelea ikiwa ni pamoja na kukarabati njia hiyo
ya kusambazia umeme kwa kuimarisha maungio,kubadilisha nguzo zilizooza na
kukata matawi ya miti yanayoizonga njia hiyo.
Pia ujenzi wa njia mpya
unaendelea ili kuhamisha wateja wa kisarawe na Gongo la Mboto kupata umeme
kupitia kituo cha Ilala.Mikakati ya muda mrefu ni pamoja na kushughulikia
upatikanaji wa transfoma kubwa ya Kipawa na upanuzi wa kituo hicho.
Kwa msaada na matukio ya dharura tafadhali piga simu namba
zifuatazo:-
022 213 3330, 0784 768586, 0715
768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715 76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya
Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 001066 ofisi ya
wilaya ya viwandani. Nama za kituo cha huduma kwa wateja (Call
centre numbers) 2194400 au 0768 985 100
Shirika
linasikitika kwa usumbufu wowote unaojitokeza kutokana na tatizo hili.
Imetolewa
na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO
Makao Makuu
Tanesco pls help,umeme unekatika hapa home tangu jana naomba msaada 0772 88 33 88
ReplyDelete