Wakarabati kituo kidogo cha kupoza umeme cha
Ilala kwa pamoja.
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Usafirishaji
Mwandisi Decklan Muhaki, akijadili jambo na
Mmoja wa Wataalamu toka JICA |
JICA, wakala
wa Japan katika kusaidia nchi za Afrika katika kuzijengea uwezo kimaendeleo. Imekuwa
na ushirikiano mzuri na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), Ambapo wamekuwa wakilisaidia shirika la TANESCO katika
kuwajengea uwezo wataalamu wake katika
kuboresha utendaji kazi wao.
JICA wamesaidia katika kuboresha mitaala ya masomo katika chuo cha Tanesco, ambacho kinatoa mafunzo ya kujiendeleza kwa mafundi Mchundo na Wahandisi.
Tarehe 25 na
26 mwazi uliopita JICA wakishirikiana na TANESCO walifanya ukarabati kituo
kidogo cha kupoza na umeme cha Ilala na kupita njia zote za kusambazia
umeme zinazotokea katika kituo hicho ili kurekebisha na kuweka sawa, hii ilikuwa
katika kutatua matatizo ya dhararu ya kukatika umeme yanayotokana na uchakavu
wa miundombinu ya umeme.
Mimi ni mkazi wa Dar eneo la moshibaa kwa Diwani. Sass ni zaidi ya siku 7 tunapata shida ya umeme Kupatwa mara kwa Mara kwa siku moja zaidi ya mara tatu. Pia umeme unaporudishwa unakuwa unaanza sana na kuwa na madhara ya aina mbili 1. Kuunguza vifaa Mimi king'amuzi, TV na pump ya maji vimeathirika
ReplyDelete