Mwishoni mwa wiki walikutana na waandishi wa habari katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, pia wameshakutana na Ujumbe wa ubalozi wa Norway, Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), EWURA na Chama cha wafanyakazi wa Viwanda na Biashara (TUICO) TANESCO ilikupata picha halisi ya TANESCO inavyooneka mbele ya jamii.
Nia haswa ya kukutana na wadau wa TANESCO ni kuona ni jinsi gani kampuni hiyo inavyoweza kushirikana naTANESCO katika kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Kampuni hiyo imemekuwa na ushirikiano na TANESCO hasa upande wa uboreshaji wa gridi ya Taifa kutoka mwaka 2008, ambapo moja ya miradi waliyosaidia ni kuwajengea uwezo mafundi wa TANESCO kwa kubadilishana ujuzi katika kuboresha gridi ya taifa Kaskazini Mashariki inayoanzia Chalinze- Hale-mpaka Arusha.
Njia hiyo ilikuwa na matatizo ya kiufundi kwa muda mrefu kwa kuakati umeme mara kwa mara lakini kwa sasa tatizo hilo limekwisha. Hivyo ushirikiano huo kwa namna moja au nyingine utaleta manufaa si kwa TANESCO tu bali hata kwa taifa.
Wawakilishi hao wanaongozwa na Makamu Rais wa Kampuni hiyo anayeshughulikia masuala ya kimataifa Bw.Tor Inge Akselsen
Maafisa
wa Statnett, wakiongozwa na Afisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud, wakiongea na Waandishi Habari wa Magazeti mbalimbali na Tv katika Hotel ya Serena. |
Maafisa wa Statnett wakisikiliza jambo toka kwa Mtangazaji wa Capital Tv Bw. Frank Morandi (wa pili kutoka kushoto) |
Mtangazaji wa Capital Tv, Bw. Frank Morandi (wa kwanza kulia),
Bw. Anders Moe kutoka Statnett, wakimsikiliza Bi. Badra Masoud hayupo pichani |
No comments:
Post a Comment