Hii ndio Transifoma iliyoharibika |
Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO linapenda kuwaomba
radhi wateja wake wote wanaoishi maeneo ya Upanga Mashariki, Eneo la Sea View
,Eneo la kituo cha polisi Daraja la Salender ,Hospitali ya Agakhan
, Mtaa wa Azikiwe, Mtaa wa Mkwepu, Mtaa wa Makunganya, Bilicana
Club, Maeneo yaliyoko kando kando ya barabara ya Bibi Titi, Mahakama ya Kisutu
,Maktaba kuu ya Tanganyika, NSSF, DIT-Chuo cha ufundi, Upanga Magharibi, Maeneo ya ofisi za
zima moto, Diamond Jubilee,Hospitali ya Tumaini , JWTZ Upanga,Hoteli ya Movenpik Serena , Barcklays
House na maeneo yanayoizunguka kwa tatizo la kukosa umeme kuanzia tarehe
06/03/2012 jioni hadi tarehe 9/03/2012 kutokana na kuharibika kwa
transfoma kubwa iliyopo katika kituo chetu cha City Centre cha kusambazia umeme
kwenye maeneo hayo kilichopo mkabala na mahakama ya kisutu.
Kazi ya dharura ya kurejesha umeme maeneo hayo ilikamilika
tarehe 09/03/2012 majira ya saa tisa usiku.
Uongozi
wa mkoa wa Ilala pamoja na uongozi wa Shirika kwa ujumla unaomba radhi na
kuwapa pole wateja wote kwa usumbufu wote walioupata kutokana na tatizo hili.
Kwa
msaada na matukio ya dharura tafadhali piga simu namba :
022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715
76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68
ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 001066 ofisi ya wilaya ya viwandani. Nama za
kituo cha huduma kwa wateja( Call centre
numbers) 2194400 au 0768 985 100
Imetolewa
naOfisi ya Uhusiano
TANESCO
Makao
Makuu.
Pamoja na jitihada zenu, tunawaomba muangalie kwanini umeme haupo stable yaani kua low voltage na high kila dakika tano hivi. Vifaa vinaweza kuharibika.
ReplyDelete