May 2, 2014

TANGAZO

TAHADHARI KWA WATEJA JUU YA KUIBUKA KWA WIMBI LA “VISHOKA- MATAPELI” MAENEO MBALIMBALI NCHINI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake kote nchini kuwa, kumeibuka wimbi la watu wanaojifanya kuwa ni wafanyakazi wa TANESCO. Matapeli hao wana vitambulisho vya uongo na unifomu za wizi.
Matapeli au Vishoka hao huja kwa nia ya kukagua mita ya mteja na humdanganya mteja kuwa mita yake imechezewa.
Baada ya ukaguzi huo wa kitapeli, wanaondoka na “Cut Out” kifaa cha kuruhusu umeme kuingia ndani ya nyumba. Baadae humpigia mteja na kumdanganya kuwa gharama za umeme ulioibiwa ni kubwa na wanaweza kuwapunguzia deni hilo kwa mteja kutoa kiasi fulani cha pesa la sivyo watamfikisha kwenye vyombo vya sheria.
TANESCO inawaomba wateja wake wote kote nchini kutokukubali utapeli huo na kwamba si Shirika wala mfanyakazi wake, anaruhusiwa kupokea pesa ya mteja kwa malipo yoyote yale nje ya Ofisi za TANESCO. Kwa vyovyote vile, mteja hata kama anadaiwa ahakikishe kwamba anakwenda kulipia deni au malipo yake kwenye Ofisi za TANESCO na kupewa risiti iliyochapishwa kwa kompyuta.
Isaidie TANESCO kuwakamata “Vishoka – Matapeli” hawa.
TOA TAARIFA OFISI YA SERIKALI YA MTAA, OFISI YOYOTE YA TANESCO, KITUO CHA POLISI AU TUPIGIE SIMU NAMBA: +255 022 2451130/38,
AU +255 768 100:  022 219 4400 AU TUANDIKIE KWENYE TWITTER YETU www.twitter.com/tanescoyetu
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO – TANESCO MAKAO MAKUU

2 comments:

  1. JAMANI UMEME MNATULETEA LINI CHIDACHI WEST MANICIPAL YA DODOMA KILOMETA TANO KUTOKA MAKAO MAKUU YA NCHI HATUNA UMEME,MAENEO YAMEPIMWA TUNA HATI KALENDA SAIZI MWAKA NA NUSU UNAPITA NI DANADANA TU.

    ReplyDelete
  2. KILA UKIENDA TANESCO WANASEMA HAWANA NGUZO MWAKA NA NUSU SASA HAKUNA UMEME TUKO GIZANI KWELI JAMANI TANESCO MKO KWA AJILI YA KUPANUA HII HUDUMA.

    ReplyDelete