November 5, 2014

KUNATAARIFA YA KUUNGUA TRANSFOMA

Kuna taarifa kwamba transfoma  ya nyumba za serikali opposite na Ubalozi wa Kenya limelipuka hivyo kusababisha hitilafu kwenye kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Oysterbay. Baadhi ya njia za kutoa umeme kwenye kituo hicho  nazo zimekata kwa sababu za kiusalama.

Maeneo yanayokosa umeme ni Oysterbay yote, Namanga, St.Peter, Kinondoni,, Adda Estate na Mkwajuni.

Mafundi wameshaanza  kushugulikia tatizo tatizo hilo.

Tutaendelea kuwafahamisha na jitihada zinafanyika kuridisha umeme.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
                       Tanesco Makao Makuu

No comments:

Post a Comment