November 2, 2014

KWA WATEJA WETU WA MKOA WA ILALA

TRANSFOMA LA 7.5MVA GONGOLAMBOTO SUBSTATION LINAVUJA MAFUTA NA LIMEZIMWA UMEME KWA DHARURA ILI KUSHUGULIKIA TATIZO HILI.

MAENEO YATAKAYOKOSA UMEME NI GONGOLAMBOTO, UKONGA, ULONGONI, PUGU,KISARAWE,KIPUNGUNI,CHANIKA, na MAJOHE.

MAFUNDI WA KARAKANA KUU YA UMEME TAYARI WAKO ENEO LA TUKIO na TAYARI WANAHAMISHA TRANSFOMA NYINGINE KUBWA YA 15MVA KWA AJILI YA KUBADILISHA.

Umeme utarudi baada ya kutatua tatizo hilo. Tunakadilia mpaka kesho mchana kazi hiyo itakamilika.

IMETOLEWA NA
                            OFISI YA UHUSIANO
                            TANESCO MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment