December 16, 2013

TAARIFA KWA UMMAUjenzi wa njia kubwa ya umeme ya kilo voti 400 kutoka Iringa mpaka Shinyanga na upanuzi wavipozeo umeme (Substations) vya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga

Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO imeanza ujenzi wa njia kubwa ya Umeme wa kilo voti 400 kutoka Iringa (Wilaya ya Iringa na Manispaa ya Iringa) mpaka Shinyanga (Manispaa ya Shinyanga na Wilaya ya Kishapu) kupitia Dodoma (Manispaa ya Dodoma, Wilaya ya Mpwapwa, Bahi na Chamwino), Singida (Manispaa ya Singida, Wilaya ya Singida Vijijini/ Ikungi, Manyoni na Iramba) na Tabora (Wilaya ya Igunga).

TANESCO kupitia Manispaa na Halmashauri husika imelipa fidia kwa wananchi wote waliopitiwa na njia hiyo. Baada ya kulipa fidia TANESCO imepokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaopitiwa na Mradi huo. Kutokana na malalamiko hayo TANESCO iliwatuma tena wathamini wa Mali kwenye maeneo husika kusikiliza malalamiko ya wananchi husika. Wathamini wamekamilisha ripoti zao na makabrasha ya FIDIA kwa wale wote wenye malalamiko halali na kwa sasa TANESCO ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa malipo stahiki.

Wakandarasi wa ujenzi wa njia hiyo wameishapatikana na wameanza kazi rasmi tarehe 21 Novemba, 2013. Katika kutekeleza mradi huo wakandarasi wamegawanywa kwenye maeneo matatu na wameshaanza kazi za awali za upimaji wa njia. Maeneo yaliyogawanywa kwa ajili ya ujenzi ni:-
·         Kutoka Iringa mpaka Dodoma (Lot 1) - Mkandarasi ni KEC International ya India.
  • Kutoka Dodoma mpaka Singida (Lot 2) - Mkandarasi ni Joyti ya India.
  • Kutoka Singida mpaka Shinyanga (Lot 3) - Mkandarasi ni KEC International ya India.

Kutokana na kuanza kwa kazi za ujenzi tajwa hapo juu TANESCO inapenda kuwataarifu na kuwaomba wananchi wote waliopitiwa na Mradi huo kuwa kwa sasa hawaruhusiwi kufanya shughuli yeyote zikiwamo za kilimo kwenye maeneo yaliyopitiwa na njia hiyo. Kwani kufanya hivyo kutachelewesha shughuli na kuongeza gharama za Mradi kutokana na wakandarasi kukosa maeneo ya kufanya kazi ya ujenzi.  

Pia TANESCO inawaomba wananchi wote wenye malalamiko halali kuwa wavumilivu wakati malipo yao yapo hatua za mwisho kukamilika.Imetolewa na:            OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment