October 31, 2014

KATIZO LA UMEME KWA BAADHI YA MAENEOMKOA WA KINONDONI KUSINIShirika la Umeme Tanzania TANESCO linawaarifu wateja wake wa Mkoa wa Kindondoni Kusini kuwa, kesho Jumamosi Novemba 1, 2014 kutakuwa na katizo la umeme kwa baadhi ya maeneo kuanzia saa  3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Magomeni, Ubungo, Kigogo, Mabibo, Mburahati, Tandale, Mlimani City, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ardhi, TCRA, TFDA, EPZA, Makoka, Kimara, Bonyokwa, King’ong’o, Mbezi Louis, Makabe, Goba Juu, Kibamba, Kwembe, Msewe, Changanyikeni, Viwanda vyote vilivyopo maeneo yaliyotajwa hapo juu na maeneo yote ya jirani.

SABABU:
Kujenga na kuweka nyaya mpya za Msongo wa Kilovolti 132/33 kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza umeme cha Ubungo ili kuondoa tatizo la umeme mdogo (low voltage) kwa baadhi ya maeneo.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo  0222171762 – 65, 0784271461, 0715271461,  Au Kituo cha miito  2194400 or 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na :         OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU


No comments:

Post a Comment