June 15, 2015

KATIZO LA UMEME MKOA WA KINONDONI KUSINI

Shirika la umeme Tanzania Tanesco linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa imetokea hitilafu ya umeme kwenye kituo kidogo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Magomeni leo juni 15,2015 jioni hii.
Mafundi wanafanya patrol kuchunguza tatizo ni nini.

Maeneo yatakayokosa umeme ni Magomeni yote, Kigogo, Ubungo plaza, Mlimani City na baadhi ya maeneo ya UDSM, TCRA na Law School.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakao jitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment