June 8, 2015

KUKOSEKANA UMEME KANDA YA ZIWA

KUKOSEKANA KWA UMEME KWA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa taarifa kuwa Majira ya saa 5.50 asubuhi ya leo Juni 8, 2015 kulitokea hitilafu kwenye Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera na hivyo kulazimu njia kuu ya Msongo wa kilovolti 220 kutoka Mtera kwenda Dodoma kuzimwa na hivyo kusababisha mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kukosa umeme. Njia hiyo ndio inayopeleka umeme mikoa ya Kanda ya Ziwa. Umeme ulirejeshwa mikoa hiyo ilipofika saa 6.30 baada ya kuondoa hitilafu hiyo. Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. 

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu

No comments:

Post a Comment