June 11, 2015

TAARIFASHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KWA WATUMIAJI WA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa taarifa kwa wateja wake kwamba Kampuni ya Pan African Energy (T) Ltd inayoendesha visima vya gesi Songosongo imezima baadhi ya mitambo yake kwa sababu ya hitilafu kwenye mfumo wa gesi.

Wakati kazi ya matengenezo ya kurekebisha hitilafu hiyo ikiendelea, kunaweza kujitokeza usumbufu kwa baadhi ya wateja hadi kazi hiyo itakapokamilika.

Kwa taarifa zilizotolewa na Kampuni ya Pan African Energy (T) Ltd, kazi hiyo inatarajiwa kukamilika jioni ya leo.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:   Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU 


No comments:

Post a Comment