June 2, 2015

KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NCHINI

Shirika la umeme nchini linapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijaamii kwamba "Mkurugenzi wa TANESCO"alikuwa miongoni mwa wajumbe 17 wanaodaiwa kuandaa mojawapo ya mikutano ya kisiasa katika hotel ya Kibo Palace Jijini Arusha.Hata hivyo taarifa hiyo imetaja tu "Mkurugenzi wa Tanesco"hivyo kufanya iwe vigumu kumjua mkurugenzi anaetajwa kwenye taarifa hiyo ni nani kwani kiongozi mkuu wa TANESCO hujulikana kama Mkurugenzi Mtendaji.

Kama taarifa hizo zilimaanisha Mkurugenzi Mtendaji basi taarifa hizo si sahihi.

Siku ya tarehe 29 Mei 2015 inayotajwa katika taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji alikuwa na mkutano na wafanyakazi wa Makao Mkuu na wa Mikoa ya Dares Salaam na Pwani kuanzia saa 7 hadi 12 jioni,uliofanyika Ubungo Dar es Salaam.Hivyo asingeweza wakati huo huo kuwepo Arusha.Kesho yake tarehe 30 Mei 2015 alisafiri kikazi nje ya nchi ambako yupo hadi sasa.

Mkurugenzi wa TANESCO kama mtumoshi wa Umma anaongozwa na kanuni za utumishi wa Umma zinazo mtaka asijihusishe kwa namna yoyote  na masuala ya siasa hivyo asingeweza kufanya hivyo kwani ingekuwa kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma.

Ikumbukwe TANESCO ni Shirika la kiufundi na lipo kwa manufaa ya watanzania wote.Mkakati wa Shirika kwa sasa,ambao Mkurugenzi Mtendaji ndiye msimamizi wake,ni kushughulikia changamoto za umeme nchini,kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika na kulifanya shirika kujiendesha kwa ufanisi zaidi kwa manufaa ya Taifa.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment