Wateja wetu mara nyingi wanakimbilia kulaumu Tanesco inapotokea mali au vitu kuungua.Ukweli ni kwamba si sahihi kukimbilia kulaumu kabla ya uchunguzi kwani unawafanya watu waamini uongo.Umeme unapokatika ukirudi hautakiwi uunguze vifaa vya mteja.Na huwa unaviwango vyake.
Umeme tunapowapelekea wateja hautakiwi uzidi wala upungue.Hitilafu ya moti wa umeme inaweza kutokana na mfumo wa utandazaji wa umeme kwenye nyumba au vibanda vya biashara ambapo jukumu hilo si la Tanesco.Umeme wa Tanesco unaishia kwenye mita kwenda ndani ni jukumu la mteja.
Nyumba au kifaa kikiungua ni lazima wataalam wa masuala ya moto waje wachunguze chanzo.Mara nyingi tumegundua wiring mbovu,zisizotumia wakandarasi waliosajiriwa na kutumia vishoka, vifaa duni vya umeme kuwa chanzo cha nyumba nyingi kuungua.
Kuhusu hili la soko la Mtambani wasubiri wataalam wa masuala ya moto watoe taarifa.wao sio wataalam ikigundulika ni Tanesco kuna taratibu zake za kufuata.
No comments:
Post a Comment