September 17, 2016

KATIZO LA UMEME MKOA WA ILALA NA TEMEKE

 Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linapenda kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala  na Temeke kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:      Jumamosi na Jumapili  17 & 18/09/2016
                    
MUDA:          02:00 Asubuhi- 12:00 Jioni

SABABU:     Uboreshwaji wa kituo kikubwa cha kusambaza na kupooza umeme
                      cha Ilala ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya kati kati ya jiji, Maeneo yote ya Upanga, Maeneo yote ya Kariaokoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala pamoja,  Kurasini yote, Mbagala yote, Chang’ombe yote, Kiwanda cha saruji Maweni, Wizara ya utalii, Tusiime mission, Tanzania oxygen, Ofisi ya manispaa ya Temeke, Unilever, Mkuu wa wilaya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya afya, Bandari gate pamoja  na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Ilala - 022 213 3330, 0784 768586, 0715 76 85 86 na  Mkoa wa Temeke 0712052720, 0758880155 na 0732997361, au Kituo cha Miito ya Simu - 2194400 au 0768 985 100.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza



Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment