September 16, 2016

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA SEPTEMBA 18, 2016

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya  Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Geita na Simiyu kuwa yatakosa umeme siku ya JUMAPILI tarehe 18 SEPTEMBA, 2016 kuanzia Saa 12:30 Asubuhi hadi Saa 11.00 Jioni.
Sababu ni kazi inayoendelea kufanywa na Mkandarasi anayefanya upanuzi katika kituo cha Shinyanga ili kuwezesha  usafirishaji umeme wa msongo mkubwa wa kilovoti 400, maarufu kama ‘Backbone’ kutoka Iringa kwenda Shinyanga.

Mradi huo unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini na utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
Android Smart Phone

No comments:

Post a Comment