September 17, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.
TAREHE:   19 Septemba, 2016. (JUMATATU)
MUDA:        3:00  Asubuhi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya MAKUMBUSHO (MAK 4), kwa ajili ya kuhamisha laini ya msongo 11KV na kupisha ujenzi wa laini mpya ya msongo 33KV wa kituo  kipya cha kupooza umeme cha Mwananyamala ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Mwananyamala, Makumbusho, Dawasa limited, ABB Office, Mwananyamala hospital pamoja na maeneo ya jirani.

1.LAINI YA TEGETA (TG3)
TAREHE:  20 Septemba, 2016 (JUMANNE)
MUDA:      3:00  Asubuhi  hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya TEGETA(TG3) kwa ajili ya matengenezo yatakayoambatana na ukataji miti inayogusa laini za umeme na kubadilisha nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya Bunju, Madale, Mivumoni na Mabwepande, baadhi ya maeneo ya Bagamoyo, Wazo Kisanga, Mbweni mpiji, Tegeta maeneo ya Kibo complex pamoja na maeneo ya jirani.

2. LAINI YA WAZO 2.
TAREHE:  20 Septemba, 2016. (JUMANNE)
MUDA:      3:00  asubuhi hadi 10:00 jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya WAZO 2, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili  kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Maeneo yote  ya  Goba, baadhi ya maeneo ya Mbezi juu na Salasala pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-           OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment