September 2, 2016

WATEJA 16,422 KUPATIWA UMEME KUPITIA MRADI WA UMEME VIJIJINI
 
Afisa Uhusiano na Huduma kwa mteja Mkoa wa Rukwa, Bwana Lucas Kusare akielezea matumizi ya Kifaa cha UMETA ambacho hutumika katika kuwafungia  wateja ambao hawakufanya  ‘‘warring’ katika nyumba zao, Kulia   ni Bwana Wilfred Malongo ambaye ni msimamizi wa mradi wa  REA mkoa wa Rukwa
     
Picha ya pamoja  ya watumishi wa TANESCO , Waalimu pamoja na  baadhi ya wanafunzi wa Kirando Sekondari.
Na Grace Kisyombe, 
 
 Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa Mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa itanufaika na upatikananaji wa umeme wa uhakika  kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini REA,
 Katika awamu ya pili ya mradi huu ambao unakaribia kumalizika  mwishoni mwa mwezi huu( August 2016)  jumla ya vijiji 74  vitanufaika ambapo zaidi ya kaya 16,422 zitaunganishiwa umeme,  

Akihamasisha wananchi kuunganishiwa umeme , Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja , Mkoa wa Rukwa , Bw. Lucas Kusare alisema , Shirika la umeme Tanzania, kwa kushirikiana na wakala wa umeme vijinini  lina lengo la kumuwezesha kila mwananchi kuwa na huduma ya umeme katika kaya , hususan maeneo ya vijijini ,hali ambayo itafanya  wananchi waweze kujikwakwamua kiuchumi kutokana na ukweli kwamba umeme unarahisisha shughuli nyingi za kiuchumi . 


Naye Afisa uhusiano   Bi Grace Kisyombe  akizungumza na wananchi katika mikutano hiyo alisema Hii ni fursa pekee ambayo Serikali imetoa kwa kuifadhili miradi ya umeme vijijini ili wananchi wapate huduma ya umeme ambayo ni muhimu kwa maendeleo yao, hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inaelekea kuwa na uchumi wa viwanda , ni vema kila mwananchi katika kaya awe na huduma ya umeme ambayo itamuwezesha mwananchi mmoja mmoja au vikundi kuanzisha viwanda vidogo ambayo vitawawezesha kujipatia kipato , pia alisisitiza kuwa gharama za kuunganishiwa umeme katika miradi hii ya umeme vijijini ni nafuu sana , kwani  mteja ambaye atahitaji kuunganishiwa umeme wa njia tatu (three phase )  atalipia shilingi 139,120/=  tofauti na wakati ambapo miradi hiyo itakuwa imekamilika na kukabidhiwa kwa TANESCO , ambapo taratibu za malipo za shirika zitatumika ambapo itampasa mteja huyo kulipa gharama ya zaidi ya shilingi laki tisa kupata umeme huo wa njia tatu. Na kwa wateja watakao taka kuunganishiwa umeme kwaajili ya matumizi ya kawaida ya majumbani  wao  katika kipindi cha mradi watatakiwa kulipia kodi ya ngezeko la thamani ( VAT ) ambayo ni sawa na sahilingi 27,000/= pekee.        

No comments:

Post a Comment