September 6, 2016

Mkoa wa Kinondoni Kaskazini





                                         SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

                                                                



 
KATIZO LA  UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:   7 Septemba, 2016 (JUMATANO)
MUDA:       3:00  Asubuhi hadi  10:00 Jioni
SABABU:   Kuzimwa kwa laini ya Bahari Beach (BB1), kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

 MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Kondo village, Bahari beach, Ununio, Rasi Kilomoni, Bulget Hotel, Chumvini, Mbweni pamoja na maeneo ya jirani.

TAREHE:     8 Septemba, 2016. (ALHAMISI)
MUDA:         3:00 Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU:     Kuzimwa kwa kituo cha kupoza umeme cha MASAKI  kwa ajili ya kuhamisha laini ya msongo wa 11KV na kupisha ujenzi wa laini mpya ya msongo wa 33KV ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Eneo lote  la Masaki, Msasani,  Oysterbay  pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika,   toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 / 0768 985 100.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO,                              
                        TANESCO - MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment