October 31, 2014

KATIZO LA UMEME KWA BAADHI YA MAENEOMKOA WA KINONDONI KUSINI



Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linawaarifu wateja wake wa Mkoa wa Kindondoni Kusini kuwa, kesho Jumamosi Novemba 1, 2014 kutakuwa na katizo la umeme kwa baadhi ya maeneo kuanzia saa  3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Magomeni, Ubungo, Kigogo, Mabibo, Mburahati, Tandale, Mlimani City, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ardhi, TCRA, TFDA, EPZA, Makoka, Kimara, Bonyokwa, King’ong’o, Mbezi Louis, Makabe, Goba Juu, Kibamba, Kwembe, Msewe, Changanyikeni, Viwanda vyote vilivyopo maeneo yaliyotajwa hapo juu na maeneo yote ya jirani.

SABABU:
Kujenga na kuweka nyaya mpya za Msongo wa Kilovolti 132/33 kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza umeme cha Ubungo ili kuondoa tatizo la umeme mdogo (low voltage) kwa baadhi ya maeneo.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo  0222171762 – 65, 0784271461, 0715271461,  Au Kituo cha miito  2194400 or 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na :         OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU


October 30, 2014

TATIZO LA KUKATIKA KWA UMEME

Shirika linaendelea kuomba subira kwa wateja wake kutokana na usumbufu wa kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara kwa baadhi ya Mikoa kwa takribani siku 5 sasa.

Sababu ya kwanza ni matengenezo na ukarabati wa miundombinu yanayoendelea ya kubadilisha nguzo zilizooza na kukata matawi ya miti yanayogusa nyaya kabla kipindi cha mvua hakijaanza.

Sababu ya pili ni matengenezo kwenye visima vya gesi huko songosongo kunakosababisha mitambo ya gesi kutopata gesi ya kutosha. Matengenezo ya miundombinu hiyo ni pamoja na visima vya gesi.

October 29, 2014

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya IJUMAA tarehe 31/10/14,  kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 011:00 Jioni.  Sababu ni Matengenezo katika kituo cha Tegeta.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-

Bahari beach, Kondo village, Ununio, Ras Kilomoni, Budget hotel, Tegeta CCM, Chanika, Njia panda ya wazo factory, Tegeta masaiti, Tegeta Namanga, Boko Basihaya, Boko CCM, Boko Maliasili, Boko National Housing, Ndege beach, Mbweni Kijijini, nyumba 151 za Serikali/Mh.Magufuli, Bakili Muluzi school, kwa Kala mweusi, Mbweni Mpiji, Wazo quorters, Dogodogo centre, uwanja wa Nyuki, Ofisi ya Raisi flats. Kunduchi yote, Kunduchi Pwani, Kunduchi Recruitment Training School (RTS) of TPDF,Mbuyuni, MECCO, JKT machimbo, Tegeta darajani, Salasala kwa Mboma, Kilimahewa, Salasala Benaco, RTD Salasala, Salasala Kijijini, Green Acres school,Part of Kilongawima, Mbezi Africana, T-square bar, mbezi Majumba sita, Lugalo Salasala, Kinzudi, Goba, baadhi ya Maeneo  salasala,Wazo kwa Makamba,Wazo mji mpya, Shule ya Sekondari wazo, Mivumoni, Madale, madale scourt, Bunju, Twiga Cement ,Salasala magengeni. Lugalo Military base, Lugalo Hospital, Maeneo yote ya Kawe, NBC Kawe, 2000 Industries Ltd, Majembe Auction Mart Mwenge, Mbezi Tangi bovu, Mbezi Lyagunga, Mbezi Zawadi, Shoko, Mwenge Survey, Kituo cha Mabasi Mwenge. Mbezi bondeni, Mtaa wa Luvent, Mtaa wa  Almas, Mwl Nyerere school, Mbezi Maguruwe,simba rd, Barabara ya Chui, Barabara Aly Sykes, Mtaa wa Beach, BOT Mbezi ,TTCL Mbezi beach, Barabara ya Zena Kawawa, Kanisa la Katolikui Mbezi beach, Mbezi miti mirefu, uwanja wa walenga shabaha, Jangwani beach, Belinda, Giraffe, Whitesands, and Green Manner hotels, baadhi ya Maeneo  Kilongawima, NMC quorters. Mbezi juu, Mbezi samaki, Baraza la Mitihani Mbezi, St.Marys school mbezi, Mbezi garden, Ndumbwi, Mbezi kwa Msomali, Mbezi Makonde, Mbezi Machakani, Mbezi NSSF, Mbezi Masoko ya kariakoo flats, Mbezi Jogoo, Art Garlery, Agape Television, Kiwanda cha Maaza juice, Polypet , Interchik, na Chemi& Cotex.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo  022 2700367, 0784 768584,  0716 768584 Au huduma kwa wateja namba 2194400.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

October 27, 2014

KATIZO LA UMEME KWA MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU, MARA, TABORA NA GEITA.



SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO ) LINAWATAARIFU WATEJA WAKE WA MIKOA YA MWANZA, GEITA, SHINYANGA, SIMIYU, MARA NA TABORA KUWA KUTAKUWA NA KATIZO LA UMEME SIKU YA JUMANNE YA TAREHE 28/10/2014 KUANZIA SAA 2.00 ASUBUHI HADI SAA 12.00 JIONI.  SABABU NI MATENGENEZO KWENYE NJIA KUU YA KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA SIGINDA HADI IBADAKULI  - SHINYANGA.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
MAENEO YOTE YA MIKOA YA MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU, MARA, TABORA, NA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA GEITA HUSUSANI WILAYA YOTE YA GEITA.

TAHADHARI:
TAFADHALI USISHIKE WAYA ULIOKATIKA, TOA TAARIFA KUPITIA SIMU ZIFUATAZO:
MKOA WA SHINYANGA NA SIMIYU:     +255 282762120, 0754 520070, 0783 520070.
MKOA WA MWANZA NA GEITA: +255 28250OO90, +255 282501060,
MKOA WA TABORA:                                  +255 2802605440.
MKOA WA MARA:                                       +255 282622020, 0732298572, 0737165087.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


IMETOLEWA NA:   OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.