TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA ARUSHA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Arusha kuto kuwepo kwa umeme kwa maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:-
TAREHE: Nyakati tofuati kuanzia 09/02/2013 hadi sasa.
SABABU:
Kuanguka
kwa nguzo 7 Mererani kutokana na upepo mkali na mvua, wizi wa nyaya za
shaba eneo la Tengeru Mjini, kuibiwa kwa cable za shaba kwenye mashine
umba (transfomer) ya Njiro AGM, kuanguka kwa miti kwenye laini kutokana
na radi na mvua na hitilafu nyingine za umeme.
MAENEO YALIYOATHIRIKA:
Merarani,
Tengeru, King’ori, USA River, KIA, Wilaya ya Siha, Wilaya ya Hai,
Njiro, Njiro PPF, Njiro AGM, Lemara, Olorien, Temdo na maeneo ya jirani
Maeneo mengi yamesha rejeshewa huduma, jitihada zinaendelea kurudisha umeme katika maeneo ambayo bado hayajapata umeme.
Tafadhali:
usiguse wala kusogelea waya wa umeme uliokatika toa taarifa TANESCO Kwa
waya uliokatika (simu: 0732979280, 2506110 na 2503551/3).
UONGOZI UNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE ULIOJITOKEZA.
IMETOLEWA NA:- OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment