February 7, 2014

MKOA WA PWANI

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kumetokea katizo la umeme siku ya JUMATANO TAREHE 05/01/2014 kuanzia saa 10.00 jioni.  Sababu ya katizo ni upepo mkali ulioambatana na Mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha nguzo 11 za umeme mkubwa (HT) kuanguka kwenye laini ya msongo wa kilovoti 33 ya Chalinze.
Aidha mafundi wetu wanaendelea na kazi hiyo ya kuhakikisha nguzo hizo zinarejeshwa katika hali ya kawaida ili huduma ya umeme iweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
Maeneo yanayoathirika ni Mboga, Lugoba, Msata, Wami, Mandera, Miono na Mbwewe
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 023 2440061, 0657 108782, 0785 122020 au kituo cha kupokea miito ya simu namba 2194400 au 0768 985 100
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote uliojitokeza
Imetolewa na:- OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.                  
                         

No comments:

Post a Comment