February 21, 2014

TANESCO yapokea magari ya kisasa

Na Queen Mwashinga - DSM

     Shirika la umeme TANESCO hivi karibuni limekabidhiwa magari 14 ya kuendeleza mradi wa usambazaji umeme na Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) katika Makao Makuu TANESCO, Ubungo jijini Dar Es Salaam yenye thamani ya Dola za Kimarekani mil 3.Akizungumza katika makabidhianoMkurugenzi Mtendaji -TANESCOMhandisi Felschemi Mramba alisema magari hayo yana uwezo wa kumpandisha fundi kufanyakazi kwenye njia ya umeme au nguzo kwa urefu wa mita 13 na nusu, na kuwa matarajio ni kwamba magari hayo yatawawezeshamafundi kufanya kazi kwa ufanisi na kuboresha huduma za wateja kwa wakati.
        Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milemia tawi la Tanzania (MCA-T) Bw BernardMchomvu amesema miradi ya MCC kwa sekta ya nishati ni pamoja
na kuboresha miundombinu ya umeme katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Kigoma, Mbeya, Morogoro na Mwanza. Kukamilika kwa miradi hii kutasadia upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo hayo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa serikali
ya Marekani wa MCC Bw Karl Fickenscher ameushukuru uongozi wa TANESCO na MCA-T kwa ushirikianomzuri katika kufanyakazi pamoja na kuboresha miundombinu ili kupunguza adha ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment