July 4, 2014

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINIShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMATATU tarehe 07/07/2014 na JUMANNE tarehe 08/07/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 11:00 jioni.  Sababu ni matengenezo ya dhalula katika njia kubwa ya Umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Tarehe 07/07/14
Mbezi Tangi bovu, Mbezi Lyagunga, Mbezi Zawadi, Shoko, Mwenge Survey, Kituo cha Mabasi  Mwenge na Maeneo ya Jirani.

Tarehe 08/07/14
Tegeta, Boko, Ndege beach, Mbweni, Mbweni, Wazo, Dogodogo centre,uwanja wa Nyuki, Bunju na Maeneo ya Jirani

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.
 

No comments:

Post a Comment