July 8, 2014

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINIShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya ALHAMISI tarehe 10/07/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 11:00 jioni. Sababu ni matengenezo, Kubadilisha Nguzo zilizooza na kukata Miti  katika njia kubwa ya Umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Maeneo yote ya Mikocheni na Viwandani, Mbezi Tangi bovu, Mbezi Lyagunga, Mbezi Zawadi, Shoko, Mwenge,  Kajificheni close, St. Peters, Don Bosco, Ubalozi wa wa Indonesia, Uwanja wa Farasi,  Josho la mbwa,baadhi ya Maeneo Msasani, Ubalozi wa Nigeria, Century hotel na Maeneo ya Jirani.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.
 

No comments:

Post a Comment