August 20, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA ARUSHA






Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Arusha kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

Watakosa umeme kwa siku za Jumamosi Agosti 22, Jumapili Agosti 23, na Jumanee Agosti 24

SABABU: Kuzimwa kwa kituo cha kupooza na kusambaza kusambaza umeme cha Mount Meru na laini ya 66kV ili kupisha Mkandarasi (TEDAP) kuunganisha njia mpya ya umeme kwenye kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Njiro.

MUDA: kuanzia SAA 2:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Mkoa wote wa Arusha

Sababu za Kujengwa kwa Mradi huu wa TEDAP ni
·         Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora (Voltage improvement) na upatikanaji wa umeme wa uhakika.
·         Kuepusha kukatika  kwa umeme mara kwa mara  kutokana na vituo kuzidiwa uwezo na kuweka  ring circuit kwa maeneo ili kuwahudumia wateja pindi upande mwingine unapokuwa na hitilafu .
·         Kujiandaa na changamoto za maendeleo za ukuaji wa viwanda na ukuaji wa mji (new master plan).Mfano Satelite cities plan( Salian City, Safari city, Bondeni city  n.k) , Maendele ya viwanda hasa uwepo wa wewekezaji wa viwanda vikubwa na upanuzi wa vilivyopo mkoani Arusha. Na kwa kuzingatia sera za serikali yetu tukufu ya Awamu ya tano.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – KINONDONI KASKAZINI

No comments:

Post a Comment