August 19, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI TAREHE: 23 Agosti, 2016 (JUMANNE)


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

SAA:          3:00  Asubuhi  hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya TEGETA(TG3) kwa ajili ya matengenezo yatakayoambatana na ukataji miti inayogusa laini za umeme na kubadilisha nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya Bunju, Mabwepande, Kwa mwana one, Dawasco, Madale, Wazo
pamoja na maeneo ya jirani.


Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO,
                          TANESCO - MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment