August 25, 2016

Kifahamu kifaa cha umeme tayari (UMETA)



Umeme tayari nikafaa ambacho akihitaji mtandao wa umeme katika nyumba isiozidi vyumba viwili au kimoja, kifaa hiki nikizuri na kinafaa kwa mtu ambae hajafanya  mtando wa umeme katika  nyumba yake na endapo jamii husika imeshindwa kufanya mtandao wa umeme katika nyumba (vyumba viwili au kimoja) kifaa cha umeme tayari ni kitamfaa zaidi.
 
Kifaa hiki kina sehemu zifuatazo:- kikata umeme(Sockect Braker),swichi kubwa (main switch), njia kuu tatu,taa moja kubwa na sehemu kuu sita za kupitisha umeme kwenda maeneo usika ya nyumba yako.
Kikata umeme (Sokect Braker), hili ni eneo mojawapo liliopo katika kifaa cha umeme tayari, sehemu hii ya kikata umeme nikuu kwa kusaidia madhara au itilafu yoyote isitokee katika nyumba yako, kwamfano umeme ukija kwa wingi vifaa vya mteja haviwezi kupata athari.

Swichi kubwa (main switch), ni eneo liliopo kwenye umeme tayari ambalo linahusika na kuwasha, kuzima umeme na endapo shida yoyote itakapotokea inajizima yenyewe ili kuepusha uharibikaji wa vifaa au nyumba kuungua.

Njia tatu za kifaa hiki zinaweza kutumika kwa matumizi tofautitofauti kama ya kupikia, kupiga pasi, na nyingine nyingi. 

Mtumiaji wa kifaa hiki anatakiwa asiwe umbali wa mita 30 kutoka nguzo ya umeme ilipo na matumizi yake hayapishani na ya nyumba iliyofanyiwa mtandao wa umeme.

3 comments: