August 26, 2016

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – WILAYA YA MKURANGA.Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake  wa Wilaya ya
Mkuranga kuwa, kutakuwa na katizo la umeme siku ya kesho  JUMAMOSI 27 AGOSTI,
2016 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni. SABABU: Kubadili nguzo
zilizooza na kukata miti kwenye njia kubwa za umeme   ili kudhibiti hali ya kukatika kwa
umeme mara kwa mara.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Baadhi ya maeneo  ya  Mkuranga, Kilimahewa, Mwalusembe, Mwanambaya, Vianzi,   Vikindu, Mwandege  pamoja na maeneo ya Jirani.

.

Toa taarifa Dawati la dharura Mkoa wa Pwani Na.  0785122020, 0657108782 au  Kituo cha miito ya simu namba 2194400 au 0768 985 100.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment