August 20, 2016

TAARIFA YA KUOMBA RADHI WATEJA WA MKOA WA TEMEKE


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake wa Mkoa wa Temeke kwa katizo la umeme lililotokea usiku wa kuamkia leo Agosti 20.

SABABU: Kutoka kwa njia ya umeme ya Ilala - Kurasini

MAENEO YALIYOATHIRIKA NI:
Kurasini yote, Mtoni yote, Mbagala yote, na baadhi ya maeneo ya Temeke.

Umeme umeanza kurejea baadhi ya maeneo ikiwemo Kurasini yote.

Mafundi wanaendelea na kazi ya kuurejesha umeme katika hali ya kawaida na tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Uongozi unaombaradhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza

           
Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment