August 19, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

TAREHE: 22 Agosti, 2016. (JUMATATU)
SAA:          3:00  asubuhi hadi 10:00 jioni

SABABU: Kuzimwa kwa njia ya umeme ya Oysterbay (O4), kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Maeneo ya Kinondoni Block 41, Kinondoni Makaburini, kinondoni shamba, Hananasifu, Mkwajuni, Moscow, Vijana   pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-           OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – KINONDONI KASKAZINI

No comments:

Post a Comment