August 23, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

TAREHE:    Jumatano  24 Agosti, 2016.
MUDA:       3:00  asubuhi hadi 10:00 jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya WAZO 2, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Maeneo yote Goba, Mbezi juu, Salasala pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika,  toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO,
                          TANESCO - MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment