August 24, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

1. LAINI YA MIKOCHENI (MK2)
TAREHE:     ALHAMISI  25 Agosti, 2016
MUDA:          3:00  Asubuhi hadi  10:00 Jioni

SABABU:  Kuzimwa kwa laini ya MIKOCHENI (MK 2) wa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Sinza, Sayansi, TTCL Kijitonyama, Rose garden, TPDC, Government House Mikocheni, Kanisa katoliki la Kijitonyama, TBC television, Johanesbarg, miti mirefu, pamoja na maeneo ya jirani.

2. LAINI YA MAKUMBUSHO (MAK4)
TAREHE:   ALHAMISI 25 Agosti, 2016.
MUDA:        3:00 Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya MAKUMBUSHO (MAK 4), kwa ajili ya kuhamisha laini ya msongo 11KV ya umeme na kupisha ujenzi wa laini mpya ya msongo 33KV wa kituo  kipya cha kupooza umeme cha Mwananyamala ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Mwananyamala na Makumbusho, Dawasa limited, ABB office, Mwananyamala hospital pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika,   toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 / 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO,                              
                        TANESCO - MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment